Bajaji Mbeya: Asante Rais Samia

HomeKitaifa

Bajaji Mbeya: Asante Rais Samia

Vijana waendesha bajaji kutoka Halmashauri ya Mbeya kata ya Mbalizi wametoa pongezi na shukurani  kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha kupata mikopo ya vijana, wanawake na walemavu  iliyowasaidia kununua bajaji wanazotumia kama kitega uchumi.

Akitoa ushuhuda mmoja wa wanufaikaji wa mikopo hiyo ni dereva Medson Mbilinyi alisema mikopo hiyo kutoka kwa halmashauri imewasaidia sana katika kuendesha maisha yake huku akirudisha kidogokidogo.

“Kiukweli huu mkopo wa halmashauri toka wameanza kutusaidia tumeingia kwenye biashara ya bajaji na mpaka sasa hivi tunakwenda vizuri, tunakwenda na marejesho vizuri kabisa na pia tumeweza kubadilisha sana maisha yetu kutokana na mikopo hii ya halmashauri,”

“Kwakweli Mheshimiwa Rais wetu wa awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan hapo ulipo sisi vijana wa Mbeya kwa ujumla tunakushukuru sana kwa mipango yote ambayo umetufanyia, mikopo uliyotutolea na tunanufaika nayo sana mpaka dakika hii, tunakushukuru sana hapo ulipo Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mbilinyi.

 

error: Content is protected !!