Bandari ya Mtwara yapokea meli kubwa ya shehena

HomeKitaifa

Bandari ya Mtwara yapokea meli kubwa ya shehena

Bandari ya Mtwara imeendelea kupokea meli zaidi zinazoleta shehena ya magari na mitambo ambapo tarehe 09 Februari, 2026 meli nyingine ya MV ANA OCEAN kutoka Nchini China imetia nanga ikiwa imebeba shehena ya mabasi, malori makubwa, matela yanayokokotwa pamoja na mitambo ya ujenzi wa miradi mbalimbali jumla ikiwa ni 1,279 yenye uzito wa Tani 7,704.

Shehena hiyo ni kwa ajili ya wateja waliopo Nchini Tanzania na nyingine itasafirishwa kwenda kwa wateja wa Nchi za Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Burundi na Rwanda.

Ujio wa Meli hizo unaendelea kudhihirisha matokeo ya Mikakati ya Kimasoko ya Bandari ya Mtwara katika kuhudumia masoko ya ndani na nchi jirani zinazotuzunguka. Lengo ni kuhakikisha Bandari ya Mtwara inakuwa lango kuu la biashara kwa Ushoroba wa Maendeleo ya Mtwara (Mtwara Development Corridor).

Aidha, kupokelewa na kuhudumiwa kwa meli hizo ni uthibitisho wa uwezo wa Bandari ya Mtwara katika kutoa huduma bora, salama na kwa ufanisi mkubwa. Uwepo wa vitendea kazi vya kisasa,miundombinu wezeshi pamoja na maboresho yanayoendelea kufanyika yanaifanya Bandari hii kuwa chaguo sahihi kwa wasafirishaji na wafanyabiashara wanaohitaji uhakika wa huduma bora wakati wote.

error: Content is protected !!