Bashe aagiza kukamatwa waliotupa parachichi

HomeKitaifa

Bashe aagiza kukamatwa waliotupa parachichi

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameagiza kukamatwa kwa mmiliki wa Kampuni ya Candia Fresh pamoja na kuifunga kampuni hiyo, kwa kile alichoeleza kuwa inanunua parachichi ambazo hazijakomaa.

Bashe amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikinunua parachichi hizo changa na kisha kuzitupa katika dampo la Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Ametoa agizo hilo jana Jumanne Januari 17, 2022 katika ziara yake mkoani Njombe na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio lililoonekana kupitia video.

Pia amepiga marufuku wafanyabiashara kuchuma parachichi zikiwa changa, kwani hakuna soko linalopokea parachichi ambazo hazijakomaa.

error: Content is protected !!