Bunge lampa Makamba siku 6 

HomeKitaifa

 Bunge lampa Makamba siku 6 

Wabunge wameitaka serikali kuja na mkakati wa dharura wa kunusuru kupanda kwa bei ya mafuta, huku wengine wao wakitaka kupunguzwa kwa baadhi ya tozo kwenye mafuta pamoja na serikali kuomba mkopo wa dharura, mjadala ulioibuliwa na Mbunge wa Kilindi (CCM), Omary Kigua akitaka bunge hilo kujadili kupanda kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa.

Baada ya mjadala huo, Spika Tulia alimwagiza Waziri wa Nishati, January Makamba kuwasilisha majibu bungeni wiki ijayo Jumanne kuhusu mkakati wa muda mfupi wa serikali katika kukabiliana na dharura iliyojitokeza nchini.

“Nimewasikia wabunge kuhusu ushauri mlioutoa kwa serikali juu ya kupanda kwa bei ya mafuta. Hivyo, serikali itafanya nini katika jambo hili? Ninamwagiza Waziri Makamba siku ya Jumanne wiki ijayo aje na majibu ya namna ya kutatua jambo hili,” aliagiza Spika Tulia.

Dk. Tulia pia alisema mkakati wa muda mrefu wa serikali kuhakikisha bei ya mafuta haipandi utaelezwa bungeni siku zijazo.

error: Content is protected !!