Chanzo cha moto soko la Karume hiki hapa

HomeKitaifa

Chanzo cha moto soko la Karume hiki hapa

Baada ya Soko la Karume Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam kuteketea kwa moto na kusababisha mali za wafanyabiashara kuteketezwa kwa moto huo uliozuka majira ya saa tisa usiku wa kuamkia jumapili, Thomas Benedicto ambaye ni mfanyabiashara na mlinzi wa zamani usiku wakati tukio linatokea ameeleza chanzo cha moto ni mateja.

“Chanzo cha moto ni mateja ambao tupo nao sokoni Karume ambao wao wanajihusisha na kuuza viatu, unajua pale sokoni kuna moja ya banda ambalo wao huwa wanalitumia kutengeneza miadarati yao ambayo huwa wanatumia mishumaa kuitengeneza na siku hiyo mshumaa ulianguka na kuanza kuungua” alisema Thomas Benedicto, Mfanyabiashara na shuhuda wa moto soko la Karume.

Thomas ameeleza pia tukio lilivyoanza na njia walizotumia kuweza kudhibiti moto huo ingawa jitihada zao ziligonga mwamba na kuzidiwa na moto huo.

“Nakumbuka wakati moto unaanza mimi nilikuwepo bado sokoni sababu mimi ni moja kati ya walinzi wa siku hiyo nakumbuka sikua mbali na banda lililoanza kuungua hivyo niliitwa na kwenda kujishuhudia na kuanza kupambana kuuzima moto na nakumbuka ilibidi tukate bomba la choo cha Halmashauri na kuchukua ndoo za choo hicho ili kuweza kuuzima moto japo baadae ulituzidi nguvu” alisema Thomas Benedicto.

Meya wa Ilala, Mheshimiwa Kumbila Moto amesema kwamba zaidi ya wafanyabiashara elfu mbili wameathirikia na moto huo huku na kuongeza kwamba serikali imeunda tume ya uchunguzi ambapo majibu yanatarajiwa kutoka baada ya siku saba.

error: Content is protected !!