Njia 6 rahisi za Kuzuia Maumivu ya Tumbo kipindi cha Hedhi.

HomeUncategorized

Njia 6 rahisi za Kuzuia Maumivu ya Tumbo kipindi cha Hedhi.

Hedhi kwa wasichana au wanawake inaweza kuja na maumivu makali sana. Maumivu hayo mara nyingi hutokea chini ya kitovu na humfanya mtu au mwanamke ashindwe kufanya shughuli zake kama ilivyo ada. Hii hutokea kila mwezi, wengine hupatwa na hali hii hata zaidi ya mara moja ndani ya mwezi mmoja, na maumivu haya yanaweza kudumu kwa siku hata zaidi ya tano.

Maumivu yanaweza kusambaa hadi kwenye mapaja, nyonga na mgongo yakiambatana na kutapika kwa wengine.

Maumivu haya husababishwa na kujikunja/kujikamua kwa kuta za mlango wa uzazi (uterus) ili kujisafisha na uchafu kutoka nje ya mwiili wako. Uchafu huo ni mazingira ambayo mwili uliyandaa kwa minali ya kupokea mtoto, lakini kama mbegu ya kiume haitoingia na kuchevusha yai la mwanamke, maana yake mpango wa mimba unakuwa haupo tena, hivyo mazingira yaliyoandaliwa na mwili kwa njia asili, lazima yasafishwe kusubiri mzunguko mwingine. Kusafishika kwa kuta za mlango wa uzazi, husababisha maumivu ya makali na kutoka na damu.

Sasa ni njia zipi mtu anaweza kutumia kubaliana na hali hiyo? au unaweza kumsaidia vipi mtu anayesumbuliwa na hali hiyo?

1. Dawa za kupunguza maumivu
Zipo dawa kadhaa zitumikaza kwa kupunguza maumivu ya hedhi kama ibuprofen (Advil), naproxen au acetaminophen, (Tylenol) ambazo husaidia sana kupunguza maumivu. Dawa hizi ni nzuri, lakini inashauriwa kuongea na tabibu kabla ya kuzitumia kuepuka kupata mzio (Allergies)

2. Unaweza kulichukulia kama mzaha, lakini ni jambo la msingi sana kwa afya yako, kufanya mazoezi hata ya kutembea umbali flani, kukimbia, au kazi yoyote inayo hitaji nguvu, moyo wako husukuma damu nyingi kwa kasi zaidi katika mwili; hii husaidia kutoa kemikali nyingine inayoitwa “Endorhins” ambayo hufanya kazi kinyume na prostaglandins na kuzuia makali yake, na hivyo kuzuia maumivu ya tumbo na kuurudisha mwili katika hali ya msawazo ya kawaida. Jaribu kufanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki, kama ulikua ukisumbuliwa na maumivu haya.

3. Tumia maji ya moto
Joto husaidia kulegeza misuli ya Uterus iliyojikaza ambayo hasa ndio chanzo cha maumivu. Kuna vifaa mbalimbali vya kisasa kwa ajili ya kazi hii, kama vile ThermaCare na Bengay, ambavyo vinatumika zaidi ya mara moja. Lakini kama huwezi kuvipata hivi, usijali, tumia njia za kawaida kama kuweka maji ya moto ndani ya chupa ya plastiki na kuanza kujikanda nayo sehemu za tumboni zenye maumivu, itakusaidia ajabu!

4. Fanya masaji kwa mafuta laini
Masaji husaidia sana, masaji chini ya kitovu kwa takribani dakika 30 inaweza kusaidia kupunguza maumivu. Lakini kama unaona ni taabu kujimasaji, basi oga mwili mzima maji ya uvuguvugu.

5 . Jizuei baadhi ya vyakula kabla ya siku zako
Epuka sana matumizi ya vyakula vyenye sukari kwa wingi, mafuta, vilevi, kafeini na vyakula vyenye chumvi kwa wingi. Kufanya hivi kunaweza kusaidia kupunguza maumivu ya tumbo wakati wa hedhi.

error: Content is protected !!