Wakati huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, watu hutumia muda wao kuwatembelea ndugu, marafiki na wapendwa wao katika maeneo mbalimbali. Tofauti na miaka ya nyuma, huenda sikukuu za mwaka huu zikasheherekewa kwa namna ya kipekee kwa sababu janga la Corona (Uviko-19) hivyo tahadhari ya mikusanyiko lazima izingatiwe ili kujiweka salama.
Mambo ya kufanya sikukuu za mwisho wa mwaka 2021
- Hakikisha umepata chanjo ya Uviko- 19 hasa kama unasafiri ndani na nje ya nchi.
- Ikiwa umeenda au unashiriki sherehe, basi iswe na watu wengi na ifanyike sehemu yenye uwazi.
- Usisahau kuvaa barakoa, kunawa mikono na maji tiririka na kutumia kitakasa mikono mara kwa mara.
- Tumia msimu wa sikukuu kuwaelimisha ndugu na marafiki kuchukua tahadhari dhidi ya Uviko- 19.
- Endapo hakuna ulazima sana wa wewe kuwatembelea watu waliopo mbali, ni vyema ukabaki nyumbani kuepusha madhara yanayoweza kutokea.
Nyimbo za mwisho wa mwaka zimeshaanza kusikika huku majengo mbalimbali yakipambwa kwa miti ya kijani na mapambo ya njano na rangi zingine za kupendeza, hivyo ni vyema ukachukua tahadhari mapema uweze kusherekea vizuri sikukuu yako na kuuanza mwaka mpya salama.