Dar Group Hospital chini ya usimamizi wa Serikali

HomeKitaifa

Dar Group Hospital chini ya usimamizi wa Serikali

Serikali imechukua usimamizi wa Hospitali ya Dar Group na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametangaza kuwa Hospitali hiyo sasa itasimamiwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Hospitali hiyo itatambulika kama ‘JKCI Dar Group Hospital’.

“Tunaishukuru Wizara ya Fedha kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kutupa @wizara_afyatz kuisimamia na kuiendesha Hospitali ya Dar Group.

Nami kwa mamlaka yangu nimeiweka Hospitali hii kuwa chini ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete @taasisiyamoyo_jkci hivyo sasa itatambulika kama JKCI Dar Group Hospital. Maono yetu ni kuona Hospitali hii inatoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo kwa watoto wa umri wa chini ya miaka 15.

Hatahivyo, Huduma za matibabu mengine ya kawaida zitaendelea kutolewa katika kipindi hiki cha mpito,” amesema Waziri Mwalimu.

error: Content is protected !!