Elon Musk ainunua Twitter apanga kufanya haya

HomeTeknolojia

Elon Musk ainunua Twitter apanga kufanya haya

Bilionea Elon Musk ambaye pia ndio mmiliki wa kampuni ya magari ya umeme ya Tesla sasa hivi ndio mmiliki mwenye hisa nyingi zaidi Twitter baada ya kupata umiliki wa 9.2% .

Ingawa hajaingia hadharani na kutamka juu ya umiliki huo. Siku chache nyuma kabla ya Mkurugenzi Mkuu wa Twitter , Parag Agrawal kumtangaza musk kuwa mmoja wao na kuwa ataingia kwenye bodi ya Twitter, Musk amekuwa akiandika maudhui mbalimbali yanayoashiria baadhi ya mabadiliko anayotaka kuyafanya kwenye kampuni hiyo

Kwanza aliandika katika ukurasa wake saa saa kadhaa zilizopita na kutaka watu wapige kura kama wangependa kuwepo na sehemu ya ‘kuedit’ama kuhariri maudhui yao Twitter wanapokosea kuandika, ujumbe ambao umependwa na zaidi ya watu laki mbili.

Kabla ya tweet yake ya leo, mwezi Machi Musk aliwahi kuwauliza watu endapo wanahisi kuna uhitaji wa kuwepo kwa mtandao mwingine.

Musk anaamini kuwa bado Twitter ipo nyuma na inahitaji mabadiliko ili iweze kufika mbali zaidi ya ilipo sasa na hivyo yupo tayari kuleta mabadiliko hayo.

“Ninatazamia kufanya kazi na Parag na Bodi ya Twitter ili kufanya maboresho makubwa kwa Twitter katika miezi ijayo!” amesema Musk akijibu ujumbe wa Parag.

Baadhi ya watumiaji wa Twitter wameonesha wasiwasi juu ya umiliki wa Musk twitter wakihisi utaathiri uhuru wa watumiaji wa mtandao huo. Wengine wamefikia hadi kumwomba airudishe akaunti ya Donald Trump ambayo ilifutwa kutokana na maudhui yake kutokukubalika na wengi.

“Kwasababu @ElonMusk ndiye mwanahisa mkubwa zaidi wa Twitter, ni wakati wa kuondoa vikwazo vya kisiasa.Oh… na MRUDISHE TRUMP!” ameandika mwanasiasa wa Marekani Lauren Boebert.

error: Content is protected !!