Ugonjwa wa Homa ya Mgunda (Leptospirosis) huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kupitia uchafuzi wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji kutoka katika mkojo wa wanyama wenye maambukizi. Maambukizi ya ugonjwa huu kwenda kwa binadamu hupitia njia zifuatazo;
i. Kugusa mkojo (au maji maji mengine ya mwili) kutoka kwa wanyama wenye maambukizi.
ii. Kugusa maji, udongo, au chakula kilichochafuliwa na mkojo wa wanyama wenye maambukizi.
iii. Kunywa maji yaliyochafuliwa na vimelea vya bakteria wa ugonjwa huu
Aidha, bakteria wanaweza pia kuingia mwilini kupitia ngozi au utando wa mucous (macho, pua au mdomo) na kupitia ngozi yenye mikwaruzo. Maambukizi ya ugonjwa huu kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine hutokea kwa nadra.