Fahamu mambo matatu yatakayoboresha kilimo Tanzania

HomeKimataifa

Fahamu mambo matatu yatakayoboresha kilimo Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imeweka mikakati ya kuimarisha kilimo ili iwe mzalishaji mkubwa wa chakula Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Alisema hayo katika mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani aliposhiriki mjadala kuhusu kilimo barani Afrika.

Mjadala huo ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) na ulihudhuriwa na viongozi kutoka baranai Afrika, serikali na sekta binafsi ya Marekani hususani waliopo kwenye sekta ya kilimo.

Katika maelezo yake, Rais Samia amebainisha mikakati mitatu muhimu ya kuendeleza kilimo kama ifuatavyo:

1. Uwekezaji katika Miundombinu ya Umwagiliaji: Serikali imepanga kuwekeza katika miradi mikubwa ya umwagiliaji ili kuhakikisha ardhi nyingi zaidi inakuwa na uwezo wa kuzalisha mazao kwa mwaka mzima. Hii inalenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kupunguza utegemezi wa mvua.

2. Kuboresha Upatikanaji wa Teknolojia na Pembejeo za Kisasa: Ili kuongeza tija na ubora wa mazao, Serikali inashirikiana na wadau wa maendeleo kutoa teknolojia za kisasa na pembejeo kwa wakulima. Hii itasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kupata mazao bora yenye thamani kubwa kwenye masoko ya ndani na nje.

3. Kukuza Masoko ya Mazao ya Kilimo: Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha mazao yanayozalishwa nchini yanapata masoko ya ndani na nje, na hivyo kuwapa wakulima faida zaidi kutokana na juhudi zao.

Rais Samia ameeleza kwamba kwa mikakati hii, Tanzania inaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula barani Afrika na hivyo kuchangia zaidi kwenye usalama wa chakula katika kanda nzima.

error: Content is protected !!