Mikoa mitano imetajwa kuwa vinara wa ukataji miti hovyo na kuharibu vyanzo vya maji.
Mikoa hiyo iliyotajwa kuharibu misitu na miti asili kwa kiasi kikubwa, Pwani, Morogoro, Tabora, Lindi na Ruvuma.
Akizungumza jana Novemba Mosi, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan, amesema mabadiliko ya tabia nchi yana sura mbili, ambazo moja ni sura ya kimungu, lakini sura ya pili ni ya kibinadamu ambao ndio chanzo kikuu cha uchafuzi wa mazingira na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji.
“Upungufu wa maji Dar es Salaam chanzo kikuu ni Mkoa wa Pwani, wanakata sana miti hovyo na ndio wapo karibu na mto Ruvu,” amesema Rais Samia.