Hivi karibuni mahusiano na ndoa za watu wengi hasa vijana zimekua zikivunja huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi au kushindwa kuvumiliana katika mambo mbalimbali.
Lakini ukweli ni kwamba wapo watu ambao huchangia kwenye kuvunjika kwa mahusiano ya baadhi ya watu hivyo endapo mtaamua kuanzisha mahusiano basi wapo wafuato wanapaswa kuzingatiwa.
Marafiki wa karibu
Wengi wanawaita ‘besties’ , watu hawa wanapaswa kuepukwa kwani ndio chnazo namba moja mahusiano kuvunjika.
Endapo umegombana na mpenzi wako, rafiki yako wakaribu ndio atakua kimbilio lako wakati ambapo upo mpweke na hivyo ni rahisi sana kuhamisha hisia kwake na kuanza hata kushiriki naye tendo la ndoa, hivyo kuwa makini.
Watu wema
Hawa ni hatari zaidi kwani huwezi dhani kama anaweza kukuchukulia mchumba wako.
Mara nyingi watu hawa huwa wapole na wapo kukusaidia kwa kitu chochote kile na kufanya kwa siri hata mwenza wako asijue. Hivyo kama upo kwenye mahusiano na kuona mtu mmoja ambaye ni mwema sana kwa mwenza wako kuwa naye makini.
Ma-Ex
Yaliyopita yanapaswa kupita, kama mwenza wako aliachana na mtu lakini bado wapo kwenye mawasiliano basi unapaswa kuwa makini kwani mtu huyu anaweza kuharibu mahusiano yenu.
Kuna uwezekano mkubwa sana wakarudiana pale ambapo wewe na mwenza wako mkipishana kauli hata kidogo. Kuwa makini na ma-ex wa mwenza wako.
Marafiki
Epuka kuwa simulia kila kinachoendelea kwenye mahusiano yako kwani marafiki wanaweza kutumia taarifa hizo kuharibu kile mlichojenga na mwenza wako.
Hasa wasichana wanapenda kuwasimulia mambo wanayofanyiwa na wapenzi wao bila kujua kwamba unampa taarifa mtu ambaye baadae anakuja kukuchukulia mwanaume wako na wewe unaachwa hivyo kuwa nao makini.