Makalla: Ukimkosa mwanao nenda polisi au hospitali

HomeKitaifa

Makalla: Ukimkosa mwanao nenda polisi au hospitali

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amesema Mzazi mwenye mtoto Panya Road kuanzia jana Septemba 15, 2022 asipomuona nyumbani asihangaike akamtafute mwanae Kituo cha Polisi au Hospitali.

RC Makalla ameyasema hayo jana katika Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Zingiziwa Chanika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Pia ametangaza Kukamatwa kwa Watuhumiwa Wengi kwenye Operesheni katika Matukio ya Tabata, Kawe na Mizumuni ambapo amesema Watuhumiwa wengi ni wale waliotoka magerezani na kumaliza vifungo hivyo ametoa rai na ana imani na mahakama kuwa itatenda haki wale ambao makosa yao yana rudia rudia hukumu yao iwe kali zaidi

RC Makalla amewahakikishia wananchi wa Dar es Salaam kuwa ulinzi umeimarika baada ya kuongeza askari 300 kushughulika na Panya Road na kuwa wananchi wasiwe na hofu waendelee na shughuli zao za kujiletea maendeleo

error: Content is protected !!