Fedha za Uviko zaingiza shule 10 bora

HomeKitaifa

Fedha za Uviko zaingiza shule 10 bora

Ilikua vigumu sana kwa watu wengi kuelewa uamuzi uliochukuliwa na Rais Samia Suluhu juu ya fedha za mkopo zilizotolewa na IMF za mapambano dhidi ya Uviko-19 baada ya kuzipeleka kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali nchini badala ya kununua vifaa vya kujikinga na janga hilo.

Fedha hizo shilingi trilioni 1.3 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) zilitumika katika utekelezaji wa kutatua changamoto za elimu, afya na maji.

Moja wapo ya shule iliyonufaika na fedha hizo ni Shule ya Sekondari Ziba iliyopo wilayani Igunga mkoani Tabora ambapo vyumba vitatu vya madarasa vilijengwa na ofisi ya walimu.

Uamuzi huu wa Mhe. Rais, umewezesha shule hii kuingia kwenye orodha ya shule 10 bora kitaifa baada ya wanafunzi kufanya vizuri. 

Hapo awali, wanafunzi walikua wakisoma kwenye mazingira ambayo yalikua yakiwafanya washindwe kufanya vizuri kwenye masomo yao.

 

error: Content is protected !!