Guardiola amwagia sifa Klopp

HomeMichezo

Guardiola amwagia sifa Klopp

Klabu ya Liverpool inaongoza kwa pointi moja mbele ya klabu ya Manchester City ambapo miamba hiyo ya soka itakutana kwenye mchezo wa Ligi kuu England siku ya Jumapili.

“Ndani ya miaka minne iliyopita ni mwaka mmoja tu ndio Manchester City imekosa ubingwa, na ni mara hiyo ambayo Liverpool imechukua,” amesema Guardiola.

> Tetesi za soka Ulaya leo Oktoba 02 (Henry akosoa kauli ya Wenger, Sterling njia panda Man City)

Katika mashindano yote waliokutana kati ya Klopp na Guardiola, Guardiola amepoteza michezo 8 mbele ya Klopp ambapo rekodi hiyo inamfanya Klopp awe kocha aliyemfunga mara nyingi zaidi Guardiola  kuliko kocha yeyote.

“Hakika Klopp amenifanya niwe kocha mzuri zaidi,” amesema Guardiola. “Amenifanya nijifunze zaidi, nifikiri zaidi na kujiboresha kila siku niwe miongoni mwa makocha wazuri”… ameongeza Guardiola.

error: Content is protected !!