Bara la Afrika ni moja katika ya mabara yanayofahamika kuwa na tamaduni mbalimbali za kipekee na zenye utofauti ambapo tamaduni nyingi zinatumika mpaka sasa.
Kusini magharabi mwa Taifa la Ethiopia, linapatikana kabila la Hamar linalotambulika hasa kwa sherehe zao za urukaji ng’ombe. Watu wengi katika kabila hili ni wafugaji wanaofanya kazi nyingine za kijamii kama kuvuna asali. Kabila la Hamar ni asilimia 0.1 ya watu wote wa Ethiopia.
Urukaji wa ng’ombe (UKUKI BULA) hufanyika kama sherehe kwa vijana wadogo wanaotoka ujanani kwenda kuwa wanaume wakubwa. Hili hufanywa ili kuangalia ujasiri wa vijana hao. Mtoto wa kwanza wa kiume huwa wa kwanza kuruka ng’ombe na hunyolewa nywele na pia mwili wake huoshwa kwa michanga wakiashiria kuoshwa kwa dhambi zake huku kichwa chake kikipakwa kinyesi wakiamini kuwa kitampa nguvu kijana huyo.
Ifikapo mchana wa siku ya sherehe Wanawake na Wasichana wadogo huchapwa fimbo kama mojawapo ya mila za kabila hilo. Wao huamini kwamba maumivu atakayopata hapo ni kiashiria tosha cha uvumilivu na uaminifu kwa wanaume zao.