Saba wafariki ajalini Dodoma

HomeKitaifa

Saba wafariki ajalini Dodoma

Watu saba wamefariki katika ajali iliyotokea kwenye Mlima Kolo, Kata ya Kolo, wilayani Kondoa mkoani Dodoma leo asubuhi baada ya basi la Emigrace (T 703 DLG) lililokuwa likitokea Babati kwenda Dar es Salaam kupinduka.

Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani humo imeeleza kuwa kati ya waliofariki wanaume ni 2, wanawake ni 2 na watoto 3, huku majeruhi zaidi ya 30 wakipelekwa Hospitali ya Kondoa na wengine Babati.

Aidha, dereva wa basi hilo amekimbia, na polisi wanaendelea kumtafuta.

Taarifa za awali zinaonesha chanzo cha ajali hiyo ni kufeli kwa breki, hivyo gari likamshinda dereva na kupinduka mtaroni.

 

error: Content is protected !!