HATARI, Kutembea peku kwenye tiles si salama

HomeElimu

HATARI, Kutembea peku kwenye tiles si salama

Mazingira tunamoishi yanaweza kuwa na hatari nyingi zinazotuzunguka pasi nasi kujua. Yapo madhara ambayo tunapata kutokana na tabia zetu au mazoea na mara nyingi matokeo ya tabia zetu huchukua muda mrefu kuleta madhara, lakini pindi madhara hayo yanapojiri, basi huwa ni makubwa sana.

Tunapenda kuwa huru tuwapo majumbani mwetu, moja ya uhuru tunaouishi majumbani mwetu ni kupenda kutembea peku, lakini nikujuze, kutembea peku kwenye sakafu ngumu, tiles au hata sakafu ya mbao, ni hatari kwa afya yako.

Unyayo wa binadamu una mafuta (fat pads) ambayo humsaidia kupunguza msuguano (friction) wa mifupa tunapotembea/kukimbia. Mafuta haya pia husadia kufanya nyayo kuhimili uzito wa mwili. Mafuta hayo yanapaswa kuwa katika ujazo mzuri kila wakati ili kuzuia maumivu ya viungo kama magoti, visigino hata nyonga wakati mwingine.

Mafuta haya yanaweza kupungua ujazo kama mtu ana tabia ya kupenda kutembea peku mara kwa mara hasa katika sakafu ngumu. Ili kuepuka tatizo hili hapo baadae, basi hakikisha unavaa ‘soksi’ nzito, viatu laini kama ‘Yeboyebo’ au weka zulia laini ndani mwako ili kuzuia hali hiyo.

error: Content is protected !!