Kukua katika miaka ya 90 ilikuwa ya kutisha sana. Hatuwezi kusahau sinema kuhusu mauaji ya kiibada ambazo zilikuwa kama filamu za kutisha na mambo mengine mengi ambayo yaliweka hofu ya Mungu ndani yetu.
Hizi ni baadhi ya dhana tulziowahi ambiwa ni zakweli;
Ukimchapa mtu kwa ufagio anapoteza nguvu za kiume
Tuliwahi ambiwa kwamba ukimpiga mwanaume na ufagio basi ataishiwa nguvu zakiume na hivyo kushindwa kumpa ujauzito mwanamke lakini kumbe ni uongo.
Ukibeba mwavuli kipindi cha jua basi mvua itanyesha siku ya harusi yako
Huwenda wazazi walikua wanatumia njia hii kutuambia kwamba tuwe na matumizi mazuri ya vitu lakini kufanya tuwe makini ndio wakatuaminisha dhana hii.
Ukimruka mtu mzima akiwa amelala basi watoto wako watakua wafupi
Wazazi walikuwa wanatumia kauli hii kutufundisha heshima na adabu kwa watu waliotuzidi umri na ndio maana tukaambiwa dhana za kutisha ili tuwe na uoga.
Ukiinua mguu wakati wa kulala basi wewe mchawi
Kwa wale waliokuwa wanatabia za kulala vibaya basi msemo huu ulikua unatumika sana kwao ili waweze kujirekebisha na kweli baada ya kuambiwa huanza kulala vizuri.
Chakula kikidondoka, usiokote kwani wachawi wameshakila
Hapa bila shaka wazazi walikuwa wanatuhimiza kwamba wakati wakula tuwe makini tusidondoshe chakula chini na pia kujilinda na maradhi kwani kikishadondoka kinapata uchafu hivyo inabidi ukiache.