Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua tovuti inayoelimisha jamii kuhusu unywaji wa pombe wa kistaarabu ambayo ipo kwa lugha ya kiingereza na kiswahili.
Mkurugenzi wa Uhusiano kwa Umma wa SBL, John Wanyancha amesema tovuti hiyo ya DRINKiQ imebeba taarifa ikiwa ni namna pombe inavyoweza kuathiri mwili, inavyoingia mwilini na namna inayoathiri uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi.
“DRINKiQ ni sehemu muhimu ya mkakati wa SBL ya kuwasaidia watumiaji wa bidhaa zake na umma kwa jumla kufanya maamuzi sahihi kuhusu unywaji wa pombe,
“Tunafurahi kuona namna mafunzo kupitia DRINKiQ yanavyopokelewa na umma na Watanzania katika miaka michache ambayo tumekuwa tukiyatoa,” alisema Wanyacha.
Pia alisema, wakati baadhi ya watu wakichagua kunywa kistaarabu, wengine hawafanyi hivyo na kuongeza kuwa, kampuni ya SBL imekuwa na itaendelea kuwa mstari wa mbele kutoa elimu kuhusu unywaji wa kistaarabu kwa njia mbalimbali ikiwamo ya mtandao.