Jux azindua Rasmi duka la African Boy

HomeBurudani

Jux azindua Rasmi duka la African Boy

Nyota wa Bongo Fleva na mfanyabiashara Juma Mussa Mkambala maarufu kama Jux, ametimiza ndoto yake ya muda mrefu kwa kufungua rasmi duka lake la nguo za ‘brand’ yake ya Africa Boy liitwalo African Boy Store lililopo maeneo ya Sinza Afrika Sana Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

Watu maarufu wengi waliweza kuhudhuria katika uzinduzi wa duka hilo na kuunga mkono juhudi za Jux katika kuendeleza ndoto zake kwani kwa mujibu wake ni kitu alichokua ameanza tangu mwaka 2013 kipindi yupo masomoni China.

https://clickhabari.com/muonekano-mpya-wa-jux-hana-mpinzani/

“Nilianza kuprint t- shirt chache za mtaani kabisa nikaziandika African Boy , nikaziweka kwenye duka la dada yangu Fatma, t- shirt nakumbuka zilikua chache sana kama ishirini hivi na nilivyopost watu wengi walitaka ile t-shirt ndani ya muda mfupi ziliisha zote, nikasema basi hii nadhani ni biashara,” alisema Jux.

Moja kati ya wageni katika uzinduzi huo ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ ambaye yeye alimpongeza Jux kwa hatua hiyo huku akimtaja kama kioo kwa vijana wengine wanaotafa kuthubutu katika kutimiza ndoto zao za muda mrefu.

error: Content is protected !!