Kampuni inatafuta watu wa kulala na kuwalipa

HomeKimataifa

Kampuni inatafuta watu wa kulala na kuwalipa

Kampuni ya utengenezaji magodoro inayofahamika kwa jina la Casper nchini Marekani, imetangaza nafasi za kazi ya kulala usingizi kwa watu watakao kuwa tayari.

Taarifa kutoka kwenye kampuni hiyo zinasema, wafanyakazi watatakiwa kulala usingizi na watakapo amka wanapaswa kuandaa maudhui kwenye mitandao ya kijamii wakieleza ufahamu wao wa kulala kama walalaji waliobobea.

Watakaofanikiwa kujiunga watapata uwezo wa kuvaa pajama ( nguo za kulalia) wakiwa ofisini na kutumia bidhaa za kampuni hiyo bure.

 

error: Content is protected !!