Kardinali Protase Rugambwa amewataka Watanzani wawe tayari kujenga na kudumisha utamaduni wa upendo na mshikamano na watu wengine hata ambao si Watanzania.
Alitoa wito huo mara baada ya kusimikwa na Baba Mtakatifu Francisko kwenye uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Kuu Petro mjini Vatican.
Katika hotuba yake, Kardinali Rugambwa amewataka watanzania kujenga na kudumisha; umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa, mambo msingi yanayowatambulisha watanzania licha ya tofauti zao. Pia amewasihi waendeleze upendo na mshikamano huo hata kwa watu ambao sio watanzania.
Kardinali Rugambwa amesema kwa kuendelea kufanya hivyo kutafanya watu waweze kufurahia na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Ufalme wa Mungu hapa duniani.
Alitumia fursa hiyo kuwakaribisha watu wote wa Mungu nchini Tanzania na kusema “Nyumbani kumenoga.”
Aidha, Kardinali Rugambwa amewashukuru wote waliompongeza pamoja na kumtakia heri na fanaka katika maisha na utume wake akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Pongezi za dhati kwa Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, kwa kusimikwa rasmi na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Kardinali. Kauli mbiu ya utume wako ni “Enendeni ulimwenguni kote”, ikiakisi mafundisho ya Yesu Kristo katika Injili ya Marko 16:15, juu ya utume unaojali watu wote,… pic.twitter.com/JwbZaRiKgQ
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) September 30, 2023