Karua: Mimi ndiye Rais ajaye wa Kenya

HomeKimataifa

Karua: Mimi ndiye Rais ajaye wa Kenya

Kiongozi wa upinzani wa chama cha People’s Liberation Party (PLP), Martha Karua, amesema ana imani kuwa yeye ndiye Rais ajaye wa Kenya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.

Karua amesema yuko tayari kushirikiana na viongozi wenye maono yanayofanana na yake akisisitiza kuwa wakati umefika kwa mwanamke kuongoza taifa na kwamba yeye ndiye anayefaa zaidi kwa nafasi hiyo.

“Safari hii mruhusu mwanamke awe Rais wa Kenya na kugawa keki ya taifa, na mimi ndiye ninayefaa zaidi kwa kazi hiyo. Wakati umefika kwa keki ya Kenya kugawiwa na mwanamke, naye si mwingine bali Martha Wangari Karua,” amesema.

error: Content is protected !!