Rais wa Marekani, Donald Trump, ametishia kuishambulia Oman endapo nchi hiyo itazuia juhudi za Marekani za kufikia makubaliano na Iran kuhusu kufunguliwa kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz.
Kauli hiyo ameitoa wakati Oman na Iran zikiendelea na mazungumzo ya kukamilisha makubaliano ya usafiri wa meli katika njia hiyo muhimu ya baharini ambapo Iran imesema imefikia hatua za mwisho za makubaliano na Oman kuhusu njia mpya za meli kupita katika mlango huo.
Trump pia ameitaka Iran kujisalimisha huku akisisitiza kuwa Marekani haitakubali hatua yoyote itakayochelewesha kufunguliwa kwa Mlango wa Hormuz, ambao ni njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta na gesi duniani.


