Bodaboda kupatiwa utambulisho maalum kufuatia uhalifu wa vishandu

HomeElimu

Bodaboda kupatiwa utambulisho maalum kufuatia uhalifu wa vishandu

Kufuatia wimbi la uhalifu unaofanywa na watu kwa kutumia pikipiki maarufu kama “vishandu,” Jeshi la Polisi mkoani Tanga limesema linapanga kuweka utambulisho maalum kwa madereva wa bodaboda.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi, amesema jeshi kwa kushirikiana na viongozi wa bodaboda linandaa utambulisho maalum utakaowatambulisha madereva halali wa pikipiki na maeneo wanakofanyia shughuli zao.

Amesema hatua hiyo inalenga kurahisisha utambuzi na upatikanaji wa madereva endapo kutatokea tukio lolote, pamoja na kuwatofautisha madereva wa bodaboda na watu wanaotumia pikipiki kwa shughuli za uhalifu.

error: Content is protected !!