Atafutwa kwa mauaji ya mama na mtoto Morogoro

HomeKitaifa

Atafutwa kwa mauaji ya mama na mtoto Morogoro

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamtafuta Anderson Jackson kwa tuhuma za mauaji ya Asha Lukonge (38) mkulima na mkazi wa Kitongoji cha Muoso, Kijiji cha Ilakala Wilaya ya Kilosa pamoja na mtoto wake Ashim Mkeza mwenye umri wa miaka tisa.

Polisi wamesema marehemu waliuawa kwa kunyongwa na mtuhumiwa ambaye alikabidhiwa familia hiyo kwa ajili ya uangalizi baada ya mume na baba wa mtoto kusafiri kuelekea Kigoma.

“Chanzo cha tukio hili ni wizi wa gunia nne za mahindi zilizokuwepo ndani ya nyumba ya marehemu, ambapo mtuhumiwa aliiba na kwenda kuziuza kwa thamani ya TZS laki tatu,” limesema Jeshi la Polisi.

Aidha, Jeshi la Polisi limesisitiza wananchi kutoa taarifa juu ya matukio ya uhalifu ili hatua ziweze kuchukuliwa.

error: Content is protected !!