Kauli za wachezaji wa Morocco zilivyoibua hisia za Waafrika

HomeKitaifa

Kauli za wachezaji wa Morocco zilivyoibua hisia za Waafrika

Hivi karibuni kumeibuka mjadala miongoni mwao waafrika hasa katika mitandao ya kijamii kufuatia kauli zinazotiliwa shaka kua ni kauli za kibaguzi kwa waafrika weusi kutoka kwa mataifa ya kiarabu hasa Morocco kufuatia kauli tata za baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa hilo mara baada ya kuiondosha timu ya Taifa ya Uhispania katika hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.

Baada ya Morocco kushinda mchezo dhidi ya Hispania na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ikiwa ni timu pekee ya Afrika iliyofanikiwa kupenya katika hatua hiyo, mshambuliaji wa pembeni wa Morocco, Sofiane Buafal alikaririwa akisema kuwa ushindi huo walioupata ni kwa ajili ya Waarabu pamoja na Wamorocco.

Katika hatua nyingine, kiungo mshambuliaji tegemezi wa Timu hiyo ya Taifa la kaskazini mwa Afrika, Hakim Ziyech anayecheza katika club ya Chelsea ya Uingereza amesisitiza kwamba Morocco haiko kwa ajili ya Taifa ama watu wengine wowote lakini kwa atakayevutiwa nao basi wanakaribisha. “

“Sisi tunapigania taifa letu sio Afrika kama watu wengi wanavyofikiri, tunataka taifa letu lifanye vizuri hayo mengine yatakuja baadae, ila kama kuna mashabiki wanataka kutushabikia basi wanakaribishwa” alisema Ziyech. 

Hata hivyo kauli hizo zimepokelewa kwa hisia tofauti na waafrika weusi mitandaoni, wengi wakiwashutumu wachezaji hao na taifa la Morocco kuonyesha wazi cheche za ubaguzi na kujitenga na waafrika wenzao huku wachache wakiamini kua wachezaji hao wapo sahihi kutokana na ukweli kwamba mashindano hayo ya kombe la dunia yanaohusisha mataifa na sio mabara, hivyo wapo sahihi kusema wanawawakilisha wa Morocco kwanza kabla ya Afrika kama bara.

error: Content is protected !!