Kuandika wosia sio uchuro

HomeKitaifa

Kuandika wosia sio uchuro

Wizara ya Katiba na Sheria imeiagiza Wakala wa Usajili, Ufilisia na Udhamini (RITA) kukusanya maoni kwa wananchi ya nini kinachosababisha wananchi kuwa na mwamko mdogo huo kwenye suala la kuandika wosia.

Mary Makondo, Katibu mkuu wa wizara hiyo amesema hayo wakati akifungua Kikao cha wadau kujadili utoaji huduma bora na endelevu kilichowashirikisha watu kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

“Bado kuna baadhi ya Watanzania ambao wanaamini kwamba kuandika wosia ni uchuro, sio kweli. Unapoandika wosia inasaidia kuweka vitu sawa hata kama ni mali na kufanya hivyo kunachangia kuondoa migogoro kwenye familia, kwa hivyo ninashauri watu kuondokana na imani hizo, waandike waosia, na tumewaagiza RITA wafanye tathmini ya kina na watupe mrejesho wa yale yanayosababisha watu wasiandike,” alisema Makondo.

 

error: Content is protected !!