Leo katika historia: Beijing inachaguliwa kuwa Mji Mkuu wa China

HomeElimu

Leo katika historia: Beijing inachaguliwa kuwa Mji Mkuu wa China

Mwaka 1962: Marekani iliiuzia Israel makombora ya kivita ya kutungulia ndege. Marekani ndiyo nchi yenye nguvu kubwa kijeshi duniani na imekuwa na ushirikiano na Israel kwa muda mrefu.

Tarehe kama ya leo mwaka 1949, Beijing, mji wenye jamii kubwa ya watu ulichaguliwa rasmi kuwa Mji Mkuu wa China. Mji wa kihistoria wa Beijing unapatikana Mashariki mwa nchi hiyo na unahesabiwa kuwa moja ya vituo vikubwa vya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni nchini China.

Mwaka 1940: Ndege 55 za Mjerumani zilizokuwa zikipita katika anga la Uingereza zilitunguliwa na wanajeshi. Ujerumani na Uingereza zilikuwa mahasimu na mashambulio hayo yalichochea Vita ya Pili ya Dunia.

Mwaka 1983: Kiongozi wa chama cha wafanyakazi cha Afrika Kusini, Curnick Ndlovu aliachiwa huru baada ya kufungwa kwa miaka 19. Serikali ya Afrika Kusini wakati huo ilipinga harakati za watu Weusi kudai haki zao.

error: Content is protected !!