Siku kama ya leo mwaka 1957: Umoja wa Jamhuri ya Kisovieti (USSR) walirusha Satelaiti ya kwanza angani kwa utaratibu huo zama za udhibiti wa anga zikawa zimeanza. Satelaiti hiyo iliyopewa jina la Sputniki 1 ilizunguka dunia mara 1400 kwa siku 92 na kwa mara ya kwanza ikafikisha ujumbe wa radio kutoka angani kuelekea ardhini.
Mwaka: 1537 Biblia ya kwanza kamili kwa lugha ya Kiingereza, “Matthew Bible” ilichapishwa, tafsiri yake ilifanywa na William Tyndale na Miles Coverdale.