Maagizo manne ya Rais Samia kwa mashirika yasiyo ya kiserikali

HomeKitaifa

Maagizo manne ya Rais Samia kwa mashirika yasiyo ya kiserikali

Katika mkutano wa mashirika yasiyo ya kiserikali uliofanyika leo Dodoma ambapo Rais Samia Suluhu Hassan amehudhuria kama mgeni rasmi, ambapo pamoja na kuwapongeza na kutambua mchango wa mashirika hayo katika maendeleo ya Taifa, ameyataka kufanya yafuatayo:

1. Ameyataka yajitahidi kuoanisha mipango yao na mipango ya taifa ili kusaidia serikali kufikia malengo yaliyokusudiwa.

2. Kuongeza uwazi katika ufanyaji wao wa kazi kutokana na kuwepo kwa mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yaliosajiliwa lakini sio yote mpaka leo ambayo yanafanya kazi mengine hayajulikani yalipo na yanafanya nini.

3. Kupunguza utegemezi kwa wahisani wa maendeleo kwani kutokana na kubadilika kwa ajenda za dunia, wahisani nao wamekuwa wakibadili sera na mipango yao ya kutoa fedha, jambo linaloyafanya mashirika tegemezi kukosa fedha za kujiendesha kwani ajenda zao zinakuwa tofauti na ajenda za wahisani.

4. Pia ameyataka mashirika hayo yasiyo yakiserikali kufanya kazi kwa kufuata mila, desturi, tamaduni na maadili ya Tanzania.

Pamoja na hayo Rais Samia ameyasihi mashirika hayo kusaidiana serikali katika kupambana na janga la korona, na  kutumia majukwaa yao kuhamasisha watu kuhusu sensa inayotarajiwa kufanyika mwaka 2022.

error: Content is protected !!