Machinga kupewa majengo ya NHC

HomeKitaifa

Machinga kupewa majengo ya NHC

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula ameagiza kuboreshwa kwa majengo matatu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambayo yapo katika mitaa ya Mkunguni na Nyamwezi karibu na Soko Kuu la Kariakoo  ili kuweza kukidhi mahitaji ya wafanya biashara wadogo maarufu kama machinga.

“TAMISEMI waliainisha mitaa ya Tandamiti na Msimbazi kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo, lakini maeneo hayo yameonyesha kutokidhi mahitaji. Lakini tumeona majengo matatu yaliyoko mitaa ya Nyamwezi na Mkunguni, karibu kabisa na Soko Kuu la Kariakoo, yanaweza kufanyiwa mabadiliko kwa ajili ya shughuli za kuhudumia mahitaji ya machinga,” alisema Dk. Mabula.

> Hii ndio mitaa 4 iliyotengwa kwa machinga wa Kariakoo

Hatua hii ni baada ya wafanyabiashara kuandika barua Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupatiwa sehemu za kufanyia biashara kwenye majengo ya NHC yaliyoko Kariakoo baada ya serikali kuamua kuwaondoa maeneo ya barabarani, waliyokuwa wakifanyia shughuli zao.

Aidha, Dk. Mabula aliitaka NHC kulichukulia suala hilo kwa umuhimu mkubwa na haraka kutokana na changamoto zake na kusisitiza kuwa wakati hatua za utekelezaji maendelezo ya majengo yaliyoainishwa ukifanyika, ni vyema kila kitu kikawekwa ili wafanyabiashara wakaelewa mwelekeo wao.

error: Content is protected !!