Mahakama: Uamuzi wa kuwaondoa Wamasai ulikua kisheria

HomeKitaifa

Mahakama: Uamuzi wa kuwaondoa Wamasai ulikua kisheria

Mahakama ya Afrika Mashariki imesema uamuzi iliyochukuliwa na serikali ya Tanzania wa kuzingira ardhi kwa ajili ya ulinzi wa wanyamapori na kuwaondoa Wamasai ulikua wa kisheria.

Dhumuni la serikali ni kulinda eneo la hifadhi lenye kilomita za mraba 1,500 ili kuepuka shughuli za binadamu uamuzi uliopokelewa tofauti na baadhi ya mashiriki ya haki za binadamu.

Aidha, Mahakama imesema, Wamasai pamoja na mashiriki ya haki za binadamu wameshindwa kudhibitisha kuhusu vurugu walizodai zimetokea, hivyo ushaidi wa madai ya vurugu na ukatili ulikuwa ni uvumi.

 

error: Content is protected !!