Polisi Kenya wanamsaka Mtanzania aliyemuua mwenzake kisa ugali

HomeKimataifa

Polisi Kenya wanamsaka Mtanzania aliyemuua mwenzake kisa ugali

Polisi nchini Kenya wanamtafuta kijana wa Kitanzania anayedaiwa kumua mwenzake wakigombani bakuli la ugali.

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Narok, Kizito Mutoro amesema wanaume hao wawili walikua wanakula chakula cha usiku siku ya Alhamisi wakati tukio hilo likitokea.

“Imeripotiwa kwamba wakati wakila chakula cha usiku, ugomvi ulianza kati ya Mungare Busene (27) na Magige (23) walipokua wakigombea ugali,” amesema Kamanda Mutoro.

Busene alinyanyua kisu na kumchoma Magige kwenye mguu wa kushoto na kisha kukimbilia kusikojululikana.

Kamanda Mutoro anasema baada ya tukio hilo, Magige aliwahishwa katika Hospitali ya Lolgorian lakini alifariki wakati akipatiwa matibabu.

 

error: Content is protected !!