Mgombea ajinadi kuwa na nguvu za kiume

HomeKitaifa

Mgombea ajinadi kuwa na nguvu za kiume

Mgombea wa nafasi ya mjumbe wa halmashauri ya CCM wilaya ya Dodoma amewavunja mbavu wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya baada ya kuwaomba wamchague kwa sababu ana nguvu za kiume.

Mgombe huyo, Chris Madaha ametoa kauli hiyo leo Oktoba Mosi, 2022 wakati akiomba kura mbele ya wajumbe 1,344 walioshiriki mkutano huo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.

Madaha ambaye aliomba kura kupitia kundi la vijana, amesema amekamilika kwa sehemu zote na ana nguvu za aina mbili ambazo ni za kimwili na kiume.

“Ndugu wajumbe, mimi nimepewa namba mbili ambayo ni namba ya ushindi, lakini nina nguvu za aina mbili ambazo ni nguvu za kimwili na kiume, nipeni kura zetu,” amesema Madaha

 

SOURCE: MWANANCHI

error: Content is protected !!