Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amewataka wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwenye sekta ya utalii, kwa sababu ya amani na utulivu na kwamba Watanzania ni watu wenye ukarimu.
Pia amepongeza uamuzi wa Katibu Mkuu Mtendaji wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO), Zurab Pololikashvili na washiriki wake kuungana na Tanzania katika jitihada za kutunza mazingira kwa kupanda miti baada ya mkutano huo
Akizungumza leo jijini Arusha kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akifungua mkutano wa 65 wa UNWTO, Kamisheni ya Afrika, Waziri Mkuu Majaliwa, alisema Tanzania licha ya amani na utulivu pia ina maeneo mengi ya uwekezaji.