Makamba: Mfumo huu si msahafu

HomeKitaifa

Makamba: Mfumo huu si msahafu

Waziri wa Nishati, January Makamba, amesema utaratibu wa uagizaji wa pamoja wa mafuta sio msahafu,hivyo unaweza kubadilishwa wakati wowote kwa manufaa ya nchi.

Aliyasema hayo jana bungeni akichangia mjadala wa makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa mwaka ujao wa fedha.

Waziri Makamba alisema,uamuzi wa uagizaji wa pamoja wa mafuta ni maelekezo ya Bunge ya mwaka 2011, kwamba kipindi hicho wabunge kwa kauli moja walishauri uagizaji ufanyike na umekuwepo takriban miaka 10. 

“Tumepokea ushauri wa wabunge na tunaufanyia kazi ili kuuboresha mfumo huu. Mfumo huu si msahafu, unaweza kubadilishwa wakati wowote pale tunapoona kuna manufaa kwa nchi. Kikubwa ni kupata unafuu wa kupata mafuta,” alisema Waziri Makamba.

Aidha, amewataka wabunge na wananchi kama kuna mtu anajua uwezekano wa kupata mafuta kwa bei nzuri kutoka baharini basi awasilishe hoja yake na wataifanyia kazi.

“Wapo wabunge wamesema wana uwezo wa kupata mafuta huko baharini kwa bei nzuri, mtu yeyote anayeweza kuleta mafuta kwa bei nafuu, karibu sana ofisini hata leo. Hatuwezi kung’ang’ania kitu kimoja wakati kuna kitu kingine kinaweza kutusaidia,” alisema Waziri Makamba.

error: Content is protected !!