Asubuhi ni sehemu muhimu sana ya siku, kwani huamua ni namna gani siku yako itakavyokwenda. Umewahi kusikia watu wakisema, “ameniharibia asubuhi yangu,” au “sitaki ugomvi asubuhi hii,” hiyo ni kwa sababu wanajua ukishaiharibu asubuhi, ni sawa na umeharibu siku.
Kila mtu anapoamka asubuhi anatamani siku yake iende vizuri, lakini sio wote wanaofanikiwa katika hilo kwa sababu siku yako kuwa nzuri au mbaya, inategemeana na nini unafanya asubuhi.
Fanya vitu hivi kila siku asubuhi ili siku yako iende vizuri na ufanikiwe katika mipango yako;
1. Panga utakayofanya
Ni muhimu sana kujua siku itakaponza utafanya nini, hili unaweza kulifanya usiku kabla ya kwenda kulala. Sio lazima upange kwa kuainisha kila dakika utakuwa unafanya, bali unaweza kuainisha mambo makubwa utakayofanya.
2. Epuka ‘snooze’
Snoozing ni kuongeza dakika chache mbele kwenye alarm yako wakati inalia ili uweze kuendela kulala. Wataalamu wanasema unapoongeza dakika tano au 10 za wewe kuendelea kulala zitaathiri siku yako kwani zitakufanya usilale vizuri ukiwaza kuamka. Mwili huitaji dakika 90 kukamilisha mzunguko mmoja wa wewe kulala.
3. Kunywa maji
Hakikisha unakunywa walau glasi moja ya maji kila siku asubuhi, unaweza ukaongeza limao au tango. Mwili wako hutumia maji unapokuwa usingizini, hivyo kuanza na maji asubuhi kunausaidia mwili wako kurudi kwenye hali yake na kumeng’enya vizuri chakula utakachokula.
4. Tafakari (Meditate)
Ubongo hupenda wakati wa utulivu, na kuuzoesha hivyo kutaufanya ufanye kazi vizuri zaidi. Jijengee mazoea haya kila siku uamkapo asubuhi.
5. Mazoezi
Toka jasho asubuhi, na utaona matokeo yake. Mazoezi hufanya ubungo kutoa kemikali ya endorphins ambayo husaidia kupunguza maumivu, kuboreka na huongeza uchangamfu. Unaweza kukimbia, kuruka kamba, kuogelea na mengine.
6. Kaa juani
Kukaa juani asubuhi hutuma taarifa kwenye mwili wako kuwa siku mpya imeanza. Tafiti zinaonesha kuwa mwanga ndio hufanya mwili kusitisha kuzalisha melatonin, homoni ambayo huufanya kuendelea kulala.
7. Kunywa kahawa
Kahawa huufanya mwili kuchangamka na kuianza siku vizuri.
8. Kifungua kinywa
Chakula ndio sehemu ambayo mwili wako nishati. Hapa sio chakula, bali chakula sahihi. Chakula utakachokula asubuhi kitakuwa nishati kwa mambo mengine utakayofanya siku nzima. Hakikisha kifungua kinywa chako kinakuwa na aina mbalimbali za vyakula kama wanga, protini, vitamini.
9. Kaa na marafiki na familia
Tenga muda wa kuzungumza na familia na marafiki. Anza siku kwa kuzungumza na mtu ambaye anakuelewa, atakayeweka tabasamu kwenye uso wako. Kukaa na watu unaowapenda kutakuchangamsha kwa siku nzima.
10. Nenda kazini
Ukifika unapofanyia kazi, hakikisha malengo uliyoyaanisha unayatimiza kwa siku husika, na ikishindikana, uwe na sababu ya msingi kwanini.
Sio lazima ufanya mambo haya yote kwa siku moja, unaweza ukachagua baadhi ukayafanya kwa siku tofauti tofauti.