Mambo 3 ya kufanya baada ya kushiriki tendo la ndoa

HomeElimu

Mambo 3 ya kufanya baada ya kushiriki tendo la ndoa

Unafanya kitu gani pale umalizapo kushiriki tendo la ndoa? Je, unafahamu umuhimu wa kujichunguza pindi tendo hili linapoisha.

ClickHabari tunakusogezea mambo 3 ya kufanya baada ya kumaliza kushiriki tendo la ndoa ili kuhakikisha afya yako inabaki kuwa salama.

  1. Kojoa mara tu unapomaliza

Kukojoa baada ya kujamiiana kunaweza kuzuia wanawake kupata maambukizi kwenye mfumo wa mkojo (UTI). Kulingana na daktari wa mfumo wa mkojo wa Jiji la New York David Kaufman, MD, wanawake wanapokojoa baada ya kujamiiana, hutoa bakteria yoyote ambayo huenda imeingia kwenye uke wake.

Na kama ukishindwa kupata haja ndogo hakikisha unakunywa maji mengi ili uweze kwenda kukojoa.

  1. Jitakase kwa upole

Wakati unapangusa uke wako (hasa baada ya kujamiiana) epuka kutumia sabuni zenye harufu kusafishia uke. Badala yake, tumia maji ya joto na sabuni isiyo na harufu ili kusafisha uke wako polepole.

3.Angalia kondomu

Kama ulitumia kondomu hakikisha unaichunguza mara baada ya kumaliza kujamiiana. 

Lazima uiangalie. Ikiwa imepasuka, uwezekano wa kuambukizwa magonjwa ya zinaa (STD) huongezeka, pamoja na uwezekano mkubwa wa ujauzito. Hivyo unapaswa kuchua hatua haraka.

 

 

 

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!