Sio kila kinachotokea na kuendelea kwenye mahusiano yenu lazima watu wengine wa nje wayajue hasa yale mambo ya siri baina yako na mpenzi wako ukaenda kutoa nje na kumwambia rafiki yako au mtu mwingine yoyote. Kama unahisi kuna kitu hakipo sawa ni vyema ukazungumza na mwenza wako.
Yafuatayo ni mambo 4 ya kuweka siri kwenye mahusiano
1. Jinsi mnavyoshiriki tendo la ndoa
Usipende kuongea mambo yanayohusiana na jinsi wewe na mwenza wako mnavyoshiriki tendo la ndoa kwa marafiki zako au watu wako wa nje, usisema mara ngapi mnatenda tendo hilo, staili mnazotumia wala muda mnaochukua katika kufanya tendo hilo kwani kwa kufanya hivyo unakuwa unamshusha thamani na kumshushia heshima mpenzi wako.
2. Hali yenu ya kiuchumi
Kamwe usiwaeleze rafiki zako hali yenu ya kiuchumi, kwani utakapo mfata ma kumwambia tatizo lako ataishia kwenda kuwaambia na watu wengine hivyo ni bora ukalimaliza tatizo hilo na mwenza wako kuliko kuwaambia watu ambao hawatakusaidia zaidi yakukusema vibaya pembeni.
3. Dosari za mpenzi wako
Hakuna binadamu aliyekamilika, hivyo vumiliana na hali utakayo mkuta nayo mpenzi wako. Ukiona amekosea muelekeze kuliko kwenda nje na kumsema kwa rafiki zako na kuanza kutangaza mapungufu yake.
4. Ugomvi na malumbano
Ili gari liweze kwenda lazima vyuma visuguane, hata kwenye mahusiano malumbano ni jambo la kawaida na kama ikitokea mmegombana usikurupuke kwenda kutangaza kwa watu bali subiri wote mkiwa kwenye hali ya kawaida muanze kuongea na kusuluhisha ugomvi huo.