Mambo muhimu ya kufahamu kabla ya kuanza kulipa mkopo wa chuo

HomeKitaifa

Mambo muhimu ya kufahamu kabla ya kuanza kulipa mkopo wa chuo

Ukiwa chuoni maisha yanarahisishwa sana ukiwa na ‘Boom’ lakini boom hilo huja na asilimia kadhaa za mkopo kwaajili ya elimu yako ambao hupaswa kulipwa baada ya kumaliza chuo.

Yapo mambo kadhaa ya lazima kufahamu kabla ya kuanza kufanya marejesho ya mkopo wako.

Fahamu kiasi cha mkopo unachodaiwa
Watu wengi hushtuka wanapokatwa kiasi fulani cha mshahara kwaajili ya mkopo wa elimu ya juu na baadaye kuona ni sawa bila kujua jumla ya kiasi wanachodaiwa.

fuatilia kujua mwaka uliorekodiwa wa wewe kuanza kuchukua mkopo. Je! ni sahihi? Ulikuwa ukipokea mkopo wa asilimia ngapi kwa kipindi chote hicho na jumla ya deni lako. Ni lazima kufahamu yote haya.

Riba na makato ya adhabu
Unapaswa kufuatilia ni asilimia ngapi ya riba inaongezeka katika mkopo wako na ni kwaajili ya nini. Lakini pia bodi ya mkopo huwa inaongeze asilimia kadhaa ya adhabu kwa wale wanaochelewa kulipa hivyo ni vyema kujua ni kiasi gani cha adhabu unalipa na kwanini.

Utaratibu wa malipo
Fahamu utaratibu unaotumika kulipa mkopo wako. Je ni kwa benki, unapaswa kufika ofisini kwao ama watakukata moja kwa moja na itachukua muda gani kwa wewe kumaliza kulipa mkopo huo.

Kiasi cha kulipa kwa mwezi
Je! kiasi gani unapaswa kulipa ndani ya mwezi mmoja?Unaweza kurudisha mkopo wako kwa mkupuo na kami inawezekana taratibu gani zifanyike ili bodi isiendelee kukukata kimakosa hata baada ya kumaliza deni lako? Ni maswali ya kupatia majibu mapema.

Usiache kufuatilia mara kwa mara kama rekodi zako zipo sawasawa.

Kwa kawaida HESLB hukata 15% ya mshahara wako kila mwezi mara baada ya kuanza marejesho.

Ikumbukwe kuwa boom sio sehemu ya mkopo unaofanyiwa marejesho bodi ya mkopo.

error: Content is protected !!