Maofisa ugani kuvaa gwanda

HomeKitaifa

Maofisa ugani kuvaa gwanda

Wakili wa Kilimo Hussein Bashe amesema maofisa ugani wote nchini wataanza kuvaa unifomu na serikali itakuwa ikitoa mavazi mawili kila mwaka.

Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa ugawaji vitendea kazi kwa maofisa ugani, hafla iliyohudhuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma kuwa serikali inataka maafisa ugani watambulike kote nchini kama ilivyo kwa madaktari na askari.

“Tumetoa pikipiki tutao kits maalumu na tunataka wawe na vifaa maalumu vya kupimia hali ya udongo (soil testing kits). Hili litatuwezesha kuongeza tija,” amesema Bashe.

Pia amemuomba Rais Samia ikiwa itampendeza maofisa ugani watakao pokea pikipiki hizo wamilikishwe kila baada ya miaka miwili kama motisha kwao.

error: Content is protected !!