Masanja akutwa na hatia ya kuzini na mwanawe

HomeKitaifa

Masanja akutwa na hatia ya kuzini na mwanawe

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Masanja Shija (58) baada ya kumkuta na hatia ya kufanya mapenzi na mwanawe wa kike aliyekuwa chini ya miaka 18.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Nzega, Godfrey Rwekite alisema kutokana na ushahidi kukamilika, mahakama imeridhia kumuhukumu Masanja Shija kutumikia kifungo hicho cha miaka 30 jela ili liwe fundisho kwake na kwa wengine.

Kwa mujibu wa mawakili wa serikali wakiongozwa na Jenipher Mandago waliieleza mahakama hiyo kuwa Desemba 2 mwaka 2021 majira ya usiku, Masanja Shija alifumaniwa akifanya mapenzi na mtoto wake wa kike mwenye umri chini ya miaka 18 Baada ya Masanja kutiwa hatiani, mawakili hao waliomba apewe adhabu kali ili liwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye tabia ya ajabu kama hiyo.

error: Content is protected !!