Matukio ya wavamiaji katika mgodi wa Barrick North Mara

HomeKitaifa

Matukio ya wavamiaji katika mgodi wa Barrick North Mara

Tarehe 21 Septemba mwaka huu kulitokea tukio ambapo wavamiaji takribani 100 kwa njia isiyo halali walivamia eneo la mgodi wakati wa mvua kubwa.

Makandarasi wa usalama binafsi wasio na silaha walijibu kwa kujaribu kuwafukuza wavamiaji wenye silaha lakini baadaye walilioomba msaada wa Jeshi la Polisi kuwatoa wavamiaji hao.

Wavamiaji saba waliwekwa chini ya ulinzi na kulingana na uchunguzi wa awali wa polisi, baadhi yao walipata majeraha kutokana na mapigano kati yao wenyewe. Mwingine aliyepata majeraha wakati wa mapigano hayo alikutwa akiwa hana fahamu na baadaye alifariki kutokana na majeraha aliyokuwa nayo wakati akisafirishwa kwenda Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

Tarehe 22 Septemba tukio lingine lilitokea ambapo tena msaada wa polisi uliombwa kuingilia kati na wavamiaji wenye silaha wenye msimamo mkali kwa kujaribu kuzuia kuingia kwa njia isiyo halali kwenye Gena Pit. Wakati wa tukio hilo, askari mmoja alifyatua silaha yake na kumjeruhi mmoja wa wavamiaji.

Alisafirishwa kwenda Hospitali ya Musoma ambapo alifariki kutokana na majeraha yake tarehe 27 Septemba.

Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu matukio yote mawili.

 

error: Content is protected !!