Meli ya sulphur za bure kwa wananchi yakifa Mtwara

HomeKitaifa

Meli ya sulphur za bure kwa wananchi yakifa Mtwara

Meli ya BOSS7 iliyobeba viwatilifu aina ya Salfa ya unga tani zaidi ya elfu 5 imewasili katika Bandari ya Mtwara ikitokea Uturuki, ikiwa ni muendelezo wa kupokea viwatilifu hivyo ambavyo vinagawiwa bure na serikali kwa wakulima wa zao la Korosho lengo likiwa kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Kuingia kwa meli hiyo inafanya jumla ya viuatilifu vilivyoingia nchini kufikia tani 10,170 katika ya 25,000 zilizoagizwa na Serikali.

Shehena hiyo itagawiwa bure kwa wakulima baada ya wiki tatu, ikiwa lengo la kuimarisha kilimo cha zao la korosho.

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Francis Alfred amesema kuwa ugawaji wa pembejeo hizo utaongeza uzalishaji wa korosho.

“Ingawa kwa sasa mchango wa zao hilo katika pato la taifa kwa mwaka ni Sh500 bilioni, matarajio ya ongezeko la uzalishaji yanalenga kufikisha uchangiaji wa Sh1 trilioni kwa kipindi hicho” amesema.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Bandari Mtwara, Norbert Kalembwe amesema kuwa meli hiyo imebeba Sulphur zaidi ya tani 5000.

“Leo tumeshudia ujio wa meli ambayo imebeba viwatilifu ambavyo ni kwa ajili ya upuliziaji katika mikorosho “amesema.

 

error: Content is protected !!