Mama wa Muziki, Mama wa Muziki wa Taarab. Siti ni mtu wa kwanza kuimba muziki wa taarabu jukwaani kwa lugha ya kiswahili. Taarab ulikuwa muziki wa tabaka la juu, ni muziki unaopigwa kwenye kasri za wafalme na kwa watu maalumu huko Zanzibar, hakuwa muziki wa masikini. Na sharti uimbwe kwa kiarabu tu, lakini siti alivunja mwiko huo.
Siti ni Msanii wa kwanza nchi hii kunakili (record) muziki kwa lugha ya kiswahili huko Bombay India mwaka 1928. Siti alizaliwa 1880 Fumba Unguja Zanzibar – Tanzania. Familia yake ilikuwa fukara sana, aliuza udongo barabarani kabla ya kuhamia Zanzibar Mjini (Stone Town) 1911. Sauti kama ya Siti hadi hivi leo haijapata kutokea, licha ya jamii wa waarabu kuwa wabaguzi, lakini hawakubagua sauti ya Siti, walimualika kwenye sherehe zako kutumbuiza.
> Rwanda kugawa simu bure kwa Wananchi
Muziki wa Taarabu lazima uwe msomi, mwanaume wa hadhi na unayeweza kuongea kiarabu ndio uimbe, lakini siti alitumia mirindimo ileile akaimba kwa kiswahili, hadi kampuni ya Uingereza ya Gramophone ilipenda sana sauti yake, ikaamua kumpeleka sana Bombay ndio kunakili. Hatua hii ilimfanya kuwa Msanii wa kwanza kurekodi kanda (Album) na kufanya mauzo kimataifa.
Siti nyimbo zake ziliakishi maisha ya wakati huo – zilipinga matabaka, ubaguzi wa rangi, unyanyasaji, kuikosoa jamii na kupiga vita rushwa. Siti alikuwa mwalimu wa Bi. Kidude, Siti alimkosha hadi mwandishi maarufu na Baba wa Falsafa na fasihi ya Kiswahili Shaaban Robert hadi kuamua kuandikia kitabu “Wasifu wa Siti Bint Saad”.
Katika maisha yake yote, aliimba nyimbo 250, na chache ndio zimehifadhiwa nyingine zimepotea. Siti alifariki 1950. Kwa mujibu wa mwandishi Shaib Abeid bendi ya kwanza ya muziki Tanzania ilianza Zanzibar iliyoitwa ‘Nadi Ikhwaan Safaa’ mwaka 1905, Siti Bint Saad, Bi. Kidude na wasanii wengi wakubwa wa muziki Zanzibar wamepita kwenye bendi hiyo ambayo hadi hivi leo, bado ipo inaendelea kufanya kazi.