Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala ametangaza kusitishwa rasmi kwa mgao wa maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Makala ameyasema hayo jana Novemba 25, 2022 katika ziara ya kukagua hali ya maji katika Chanzo cha Ruvu chini.
“Kwa wiki mbili, tatu hali ya maji Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kulikuwa na uhaba kutokana na ukame, serikali imefanya jitihada kubwa kuondoa watu maeneo ya vyanzo kwenye milima ya Uluguru na Pwani, mvua zimeanza kuonyesha na sasa hali ya maji ni nzuri,” amesema Makala.
Alisema mtambo wa Ruvu Juu unazalisha lita milioni 196 na Ruvu Chini lita milioni 270 na kufanya kuwe na lita milioni 466.