Miradi 630 ya kampuni za India yasajiliwa kuwekeza Tanzania

HomeKitaifa

Miradi 630 ya kampuni za India yasajiliwa kuwekeza Tanzania

Miradi mipya 630 ya uwekezaji inayotekelezwa na kampuni za India yenye thamani za dola 3.68 bilioni imesajiliwa katika mwaka wa fedha 2021/2022 kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokutana na ujumbe wa Bunge la India (Lock Sabha) ulioongozwa na Spika, Om Birla, kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye yupo nje ya nchi kikazi.

Alisema hatua hiyo inatokana na jitihada za kuboresha mazingira ya uwekezaji zinazofanywa na Serikali.

Alisema Tanzania na India zina ushirikiano mkubwa wa kiuchumi na biashara na India ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na ushirkiano wa biashara unaofikia dola za Marekani bilioni 4.58 kwa mwaka 2021/2022.

 

error: Content is protected !!